• HABARI MPYA

  Alhamisi, Juni 25, 2015

  MKUDE APAA KWENDA KUJARIBU BAHATI AFRIKA KUSINI

  KIUNGO wa Simba SC, Jonas Mkude (pichani) ameondoka mchana wa leo kwa ndege ya Shirika la Afrika Kusini kwenda nchini Afrika Kusini kwa majaribio katika klabu ya Bidvest Wits.
  Tovuti ya Simba SC imeandika kwamba Mkude Mkude ameondoka akiwa na baraka zote za Klabu ya Simba,  
  Akizungumza Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Mkude amewaomba Watanzania wazidi kumwombea ili aweze kufuzu majaribio.
  Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Simba inamtakia kila la kheri Mkude kwenye majaribio yake kwenye Klabu ya Bidvest Wits huko Afrika Kusini na hili liwe fundisho kwa vijana wengine kuendeleza vipaji ili waweze kucheza mpira kwenye ligi za Nchi nyingine kubwa hivyo kukuza upeo na vipaji Zaidi katika soka”
  Mkude alizaliwa Desemba 3, 1992 Kinondoni B na kuanza soka lake akiwa mlinda mlango hadi kuwa kiungo wa kutegemewa. Aidha alianza elimu ya msingi mwaka 1998 katika shule ya Hananasif na kumaliza mwaka 2005.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MKUDE APAA KWENDA KUJARIBU BAHATI AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top