• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 23, 2015

  SIMBA SC YAAJIRI KOCHA WA MAKIPA MKENYA, ALIPIGA KAZI HADI HARAMBEE STARS

  KLABU ya Simba imefanikiwa kuingia mkataba na Abdul Iddi Salim (pichani kulia) kama kocha mpya wa makipa na anatarajiwa kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi July.
  Tovuti ya Simba SC imeandika kwamba, Salim ambaye ni raia wa Kenya pia amewahi kuwa kocha wa makipa wa mabigwa wa ligi ya Kenya Gor Mahia 2013 – 2014, vilevile amewahi kufundisha makipa wa timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars).
  Klabu ya Simba inafuraha kubwa kuingia mkataba na kocha huyu mwenye uzoefu na weledi wa kutosha, tunaamini atakuwa chachu ya mafanikio pia kunoa vipaji vya wachezaji wa Simba.
  Jana Simba SC ilimtangaza kocha wake mpya, Muingereza Dylan Kerr aliyesaini Mkataba wa mwaka mmoja. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAAJIRI KOCHA WA MAKIPA MKENYA, ALIPIGA KAZI HADI HARAMBEE STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top