• HABARI MPYA

    Thursday, June 25, 2015

    MKWASA AMERITHI ‘MARADHI’ TAIFA STARS, KAZI ANAYO HADI ANATIA HURUMA.

    Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
    NILIKUTANA na Mwandishi Mkongwe Magid Mjengwa  pale idara ya Habari maelezo,huyu jamaa anapenda sana kusoma ,yani mpaka leo bado anasoma na pia ni Mwalimu. Ni mmoja kati ya watu wanaoongea huku wakimaanisha. Ni mmoja kati ya Waandishi wakongwe na wazalendo wa Nchi hii waliyobaki.
    Kudhihirisha hilo akasema yeye amesafiri sana katika Nchi Mbalimbali lakini bila kutumia usafiri wa Ndege, Meli au gari. Sasa kasafiri vipi? Akasema amesafiri sana kwa kutumia Vitabu, yaani anasoma sana Vitabu.
    Pili, akasema Miaka fulani Taifa la India lilikumbwa na Njaa kali, wazazi wakawa wanaweka pilipili nyingi sana katika chakula kidogo wanachopata, watoto wakila wanawashwa sana na baada ya kuwashwa hunywa maji mengi kujipooza. Hivyo basi tumbo hujaa na ndiyo maana mpaka leo Wahindi hupenda Pilipili.
    Charles Boniface Mkwasa (kushoto) na Msaidizi wake, Hemed Moeocco

    Wenye mahaba makubwa na Soka wana njaa kali sana, anachokifanya Malinzi ni  kutuwekea pilipili nyingi ili tunywe maji mengi na Tumbo lijae tujione tumeshiba na tusiwaze Chakula.
    NIANZE kwa kumpa pole Mkubwa wangu  Charles Boniface Mkwasa `Master` kwa kuteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ( TAIFA STARS) Pole sana Mkuu.
    Inawezekana wengine mkanishangaa kwa kumpa pole ya thati Mwalimu huyo mzowefu na mwenye weledi Mkubwa badala ya kumpa `KONGOLE.
    Binafsi sina shaka hata kidogo na uwezo wa mwalimu huyo ambaye mpaka anapewa ajira hiyo bado ni Mwalimu msaidizi wa Timu ya Yanga.
    Uwezo wake kwa hapa Tanzania Ni mkubwa na hata Yanga walistahili kumpa kazi ya kuwa Kocha Mkuu na labda utumwa tu ndiyo unatelemaza kumuona mwenye ngozi nyeupe Ndiyo mwenye uwezo wa kila kitu jambo ambalo si sahihi bali ni utumwa tu wa kifikra.
    Matatizo yanayoiandama Timu yetu ya Taifa ni mengi na siyo tatizo moja ama mbili . Na Ndiyo pamoja na matatizo ya Mart Nooj na kuandolewa kwake bado siyo `mwarabaoni` wa tatizo linalotusibu.
    Hebu kaa `Kitako` jiulize ni Waalimu wangapi wameshaifundisha Timu ya Taifa  ya Tanzania wakaondoka wenyewe au walifukuzwa.
    Je kwa muda huo tatizo bado ni Waalimu tu? Ifike mahali tutafute suluhu ya kudumu na siyo kuwatupia `mzigo` waalimu  bila kuangalia matatizo zaidi ya Mwalimu.
    Kupewa jukumu kwa Mkwasa na Msaidizi wake mwajina wangu Hemed Morocco siyo suluhu ambayo itatufanya tufurahike kila stars inapokuwa uwanjani ingawa sina shaka na uwezo wa Waalimu hao wawili.
    Narudia tena kusema Matatizo yanayotuandama katika Soka Ni mengi sana,Mojawapo ni aina ya Wachezaji siyo wanaoteuliwa kuunda Timu ya Taifa bali ujumla wake hivyo lazima walewale wachaguliwe .
    Pili ni Ligi yetu ambayo ndiyo chimbuko la kupata wachezaji bora jinsi ilivyo,Mchezaji bora na kocha bora anavyopatikana.
    Mkwasa ameridhi wachezaji walewale mahiri wa kuiga mitindo ya Nywele,kustareheka vilabuni  na waliyokosa uzalendo.
    Ameridhi wachezaji wanaocheza michezo michache katika Ligi yao,ameridhi wachezaji wanaopumzika kwa muda mrefu katika Ligi bila kucheza.
    Ameridhi aina ya wachezaji waliyokosa `Control` na wasiyojiamini wawapo uwanjani.
    Ameridhi wachezaji wenye kuweka mbele maslahi yao bila kuweka mbele utaifa wao, ni aina ya wachezaji wanaowaza  baadaye na siyo kesho na keshokutwa .
    Ni wachezaji mahiri wa kuiga mitindo ya Nywele ya wachezaji wa ughaibuni kuliko kuiga mbinu na mitindo ya soka wawapo uwanjani.
    Ni Wachezaji wanaodhani kuwa wao ni jicho na hawapaswi kuguswa ila waguswe wanaowafundisha,Kwani wao wanafundishika? Hao hawajui lugha ya Kiingereza ,sasa wamepewa mwalimu anayeongea lugha ya Kiswahili, nacho hawajui?
    Angalia wanavyokamia mchezo mmoja na kesho ukimuona katika mchezo mwingine utatapika!
    Hivyo pamoja na Jitihada za Mkwasa na Hemed Lakini nachelea kusema Stars imezaliwa upya kutoka na aina ya wachezaji tuliyonao ingawa yapo matatizo mengine pia.
    Bao la Pil;I ililofungwa Stasra dhidi ya Uganda lilitokana na Striker wa Uganda kuambaa ambaa na mpira huku Kanavari akimkimbiza ,hatua chache kabla hajaingia katika eneo la 18 aliachia shuti kali lililokwenda moja kwa moja Nyavuni.
    Nafasi kama hiyo alipata Simon Msuva katika Mchezo huo na hakutumia vizuri alikosa goli,( simlaumu) hata akiwa na Mkwasa ataendelea kukosa. Mkwasa hafai? Au Msuva ndiyo hafai?
    Hili suala la uzalendo Ni Vyema Seikali nayo ikaingilia kati, iwachukue wachezaji wote waliyoitwa kuunda kikosi cha stars,wapelekwe kambi ya JKT angalau mwezi mmoja kwanza, wafundishwe uzalendo halaf waje kufunzwa soka kisha angalau tuanze kucheza na Somalia kwanza, Siyo Misri tena.
    Yapo Matatizo mengi kama nilivyotangulia kusema lakini hili la wachezaji kukosa uzalendo,kukosa maono ya mbele,kuridhika na kupuuza viwango vyao ni tatizo la kwanza.
    Kuna Timu inaweza kupoteza mchezo lakini ukawaopa sifa kutokana na wachezaji wake kujituma sana, hapo Ndipo ule msemo wa kukosa bahati unapijiri.
    Sasa kwa timu ya Taifa ya Tanzania kusema wamekosa bahati si `ujinga` jamani!!! Hata kushambulia na kufika langoni kwa adui ni taabu ,hiyo bahati inatoka wapi?
    Uwezo wa wachezaji wa Tanzania Ni Mdogo sana, ukijumlisha na kuweka maslahi yao mbele kuliko utaifa unapata nini? Kwa nini hawajitumi?
    Kudhirisha hilo wachezaji karibu wote ukiwauliza tatizo nini hawasemi kama tatizo ni kocha, ila wanasema aahh  bahati tu kaka hatuna`.
    Pole sana Mkubwa Mkwasa na Hemed Morocco.

    (Mwandishi wa makala haya ni mtangazaji wa Redio One na ITV, anayepatikana kwa namba +255 655 250 157 na +255 752 250 157)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MKWASA AMERITHI ‘MARADHI’ TAIFA STARS, KAZI ANAYO HADI ANATIA HURUMA. Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top