• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 27, 2015

  EL MERREIKH YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAWAPIGA 2-0 WAALGERIA KHARTOUM

  Na Mwandishi Wetu, KHARTOUM
  TIMU ya El Merreikh ya Sudan imeanza vyema hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga MC El Eulma ya Algeria mabao 2-0 katika mchezo wa Kundi B Uwanja wa El Merreikh mjini Khartoum usiku wa jana.
  Wenyeji walijihakikishia pointi tatu baada ya beki wa Eulma, Adel Namane kujifunga katika harakati za kuokoa dakika ya saba.
  Kipindi cha pili, Merreikh walifanikiwa kupata bao la pili lililodungwa na Bakri Al Madina akimalizia pasi ya Didier Libere dakika ya 60.

  Sasa Mashetani Wekundu hao wa Khartoum wanaongoza Kundi B ingawa wanaweza kushuka, kutegemea na matokeo ya Jumapili katika mchezo mwingine wa kundi hilo kati ya ES Setif na USM Alger zote za Algeria.
  Ushindi huo unaipa nafasi timu ya Diego Garzitto kwenda ugenini kifua mbele katika mchezo wa pili dhidi ya USM Alger wiki ya pili ya mwezi ujao, wakati MC Eulma watakuwa wenyeji wa Setif Julai 11.
  Kikosi cha Merreikh kilikuwa: J. Salim, Ala'a Eldin Yousif, Musaab Omer, Ragei Abdalla, Amir Kamal, A. Okrah, Ramadan Agab, D. Liberé, Bakri Al Madina, S. Jabason, F. Coffie
  Eulma: M. Ousserir, N. Oussalah, K. Bouzama, A. Maïza, A. Namane, M. Belhadi, I. Benettayeb, I. Chenihi, W. Derrardja, F. Hemitti, A. Abbès
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EL MERREIKH YAANZA VYEMA LIGI YA MABINGWA AFRIKA, YAWAPIGA 2-0 WAALGERIA KHARTOUM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top