• HABARI MPYA

    Tuesday, June 23, 2015

    NGASSA AWASILI AFRIKA KUSINI TAYARI KUANZA KAZI

    Na Prince Akbar, JOHANNESBURG
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa amewasili mjini Johannesburg, Afrika Kusini kujiunga na klabu yake mpya, Free State Stars kwa maandalizi ya msimu mpya.
    Ngassa amepokewa na gari maalum la klabu hiyo akiwa na mkewe, Radhia ‘Nish’ Enea Mngazija tayari kwa safari ya Bethlehem, yalipo makao makuu ya FS.
    Ngassa ambaye jana alifanya mazoezi na timu yake ya zamani, Yanga SC Uwanja wa Karume, Dar es Salaam alipewa ruhusa ya kuja kujiunga na timu ya taifa, Taifa Stars.
    Bahati mbaya, Ngassa aliondolewa katika kambi Stars iliyokuwa inajiandaa kwa mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda Raundi ya Kwanza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya Shirikisho la Soka  Afrika (CAF) kusema haruhusiwi kucheza kwa kuwa amekwishasaini Mkataba na timu ya Afrika Kusini, japokuwa hajaanza kuitumikia.
    Ngassa akiwa na mkewe Nish 'Shombe Shombe' baada ya kutua Johannesburg tayari kwa safari ya kilomita zaidi ya 100 kwenda Bethlehem
    Ngassa na Nish wake wakiwa kwenye ndege ya Shirika la Afrika Kusini asubuhi leo kwenda Johannesburg

    Baada ya mechi na Uganda, ambayo Tanzania ilichapwa mabao 3-0, Ngassa alirejea Dar es Salaam na wakati anasubiri kutumiwa tiketi ya kurejea kazini Bethlehem, jana aliamua kufanya mazoezi ya kujiweka fiti na Yanga SC. 
    Na baada ya mazoezi mashabiki walisukuma gari lake hadi nje yaa geti kwa furaha, wakiimba; “Tutarudisha fedha (za Free State) urudi Yanga,”.
    Alipoulizwa mwenyewe sababu za kufanya mazoezi na Yanga SC jana, Ngassa alisema; “Yanga ni timu yangu, sijaondoka kwa ubaya, naweza kurudi wakati wowote,”.
    “Nilipewa ruhusa ya kuja kuchezea timu ya taifa, bahati mbaya siku mbili kabla ya mechi na Uganda, nikaambiwa siwezi kucheza. Kwa hivyo, wakati nasubiri kutumiwa tiketi, nimeona nije kufanya mazoezi na Yanga kujiweka fiti,”amesema.
    FS walimtumia tiketi jana Ngassa na leo asubuhi amepanda ndege na mkewe Nish ‘Shombe Shombe’ kurejea kazini.
    Ngassa alisaini FS Mei mwaka huu Mkataba wa miaka minne baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka miwili Yanga SC akiiacha na ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Ngassa jana alifanya mazoezi na Yanga SC Uwanja wa Karume kujiweka fiti
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NGASSA AWASILI AFRIKA KUSINI TAYARI KUANZA KAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top