• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 24, 2015

  BUSUNGU ATUPIA MBILI, YANGA SC YAUA 3-2 KARUME

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga SC, Malimi Busungu amefunga mabao mawili timu yake ikishinda 3-2 dhidi ya Friends Rangers katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Karume.
  Yanga SC inaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na leo kwa mara ya kwanza ilicheza mechi.
  Kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm aliwaanzisha wachezaji wake wote wapya wakiwemo Malimi Busungu, Deus Kaseke na Kamara kutoka Mali dhidi ya timu hiyo ya daraja la Kwanza.
  Malimi Busungu ameanza vizuri Yanga SC akifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Friends Rangers leo

  Yanga SC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 11, mfungaji Mliberia Kpah Sherman aliyemalizia pasi ya Busungu.
  Friends Rangers walifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 25, mfungaji Mussa Juma ‘Rooney’ kabla ya Sherman kumpasia Busungu dakika ya 37 kuifungia bao la pili Yanga SC.
  Hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 2-1 na kipindi cha pili kila timu iliongeza bao moja.
  Cossmas Lewis alianza kuifungia Rangers bao lililoelekea kuwa la kusawazisha dakika ya 83 kabla ya Busungu kuifungia Yanga SC bao la ushindi dakika ya 88. 
  Pamoja na kwamba Rangers walikusanywa kusanywa tu na Heri Mzozo kwa ajili ya mechi hiyo, lakini ‘waliitoa jasho’ Yanga SC.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BUSUNGU ATUPIA MBILI, YANGA SC YAUA 3-2 KARUME Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top