• HABARI MPYA

    Monday, June 29, 2015

    CHALLENGE YAFUFUKA, ETHIOPIA WAKUBALI UENYEJI 2015 NGOMA KUPIGWA NOVEMBA ADDIS

    Mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Samatta akiwatoka mabeki wa Zambia katika mechi na Zambia Uwanja wa Nyayo Nairobi, Kenya katika Challenge ya mwisho mwaka juzi timu hizo zikitoka sare ya 1-1

    MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge sasa itafanyika Ethiopia baada ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo kuthibitisha kuwa wenyeji.
    Kombe la CECAFA Challenge linatarajiwa kuanza Novemba kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Soka Ethiopia (EFF), Junedin Basha.
    Basha, ambaye amewaomba wadau wote Ethiopia kuunganisha nguvu zao ili michuano hiyo ifanikiwe, amepania kufanya vizuri baada ya awali kujitoa kuandaa michuano hiyo mwaka jana.
    Ameandika katika akaunti yake ya Twitter, “Ethiopia itakuwa mwenyeji wa CECAFA ya 2015 mwezi Novemba. Acha wote tuunganishe nguzu zetu kufanikisha hili. Hongera!”
    Awali, Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye aliwaomba Rwanda waandae michuano hiyo kwa mwaka huu kama maandalizi yao kabla ya kuwa wenyeji wa CHAN ya 2016 kuanzia Januari 16 hadi Februari 7, lakini wakakataa.
    Kenya ndio mabingwa watetezi walioifunga Sudan 2-0 mwaka 2013 michuano hiyo ilipofanyika mara ya mwisho nchini Kenya.
    Uganda ndio mabingwa wa kihistoria baada ya kubeba taji hilo mara 13, wakati wenyeji wa mwaka huu, Ethiopia walitwaa taji hilo kwa mara ya mwisho mwaka 2004 wakiifunga Burundi 3-0 katika fainali nchini Ethiopia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHALLENGE YAFUFUKA, ETHIOPIA WAKUBALI UENYEJI 2015 NGOMA KUPIGWA NOVEMBA ADDIS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top