• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 26, 2015

  MAKOCHA WA MAKIPA LIGI KUU KUNOLEWA

  Kocha wa makipa wa Yanga SC, Juma Pondamali naye anahudhuria kozi ya makocha wa makipa
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limezitaka klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kuwasilisha majina ya makocha wao wa makipa kwa ajili ya kuatiwa mafunzo.
  Taarifa ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa TFF, Baraka Kizuguto, imesema kwamba klabu hizo zinatakiwa kuwa zimefanya hivyo hadi kufikia Jumatatu ya Juni 29, mwaka katika ofisi za shirikisho hilo, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
  TFF imeandaa kozi ya makocha wa makipa itakayofanyika kuanzia Julai 13 hadi 17 Julai, 2015 mjini Dar es Salaam na kila klabu inatakiwa kutuma jina la kocha mmoja ili ashiriki kozi hiyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAKOCHA WA MAKIPA LIGI KUU KUNOLEWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top