• HABARI MPYA

  Jumatatu, Juni 29, 2015

  ARSENE WENGER AFANYA KWELI, SASA PETR CECH NI KIPA WA ARSENAL

  KIPA Petr Cech ametambulishwa rasmi na Arsenal baada ya kocha Arsene Wenger kukamilisha mpango wake wa muda mrefu wa kumsajili.
  Arsenal imetoa kiasi cha Pauni Milioni 10 kwa Chelsea ili kumnunua mlinda mlango huyo hodari wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech.
  Kwa kuhamia Kaskazini mwa London, Cech aliyesaini Mkataba wa miaka minne, atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki.
  Mkongwe huyo anaweza akaidakia The Gunners kwa mara ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani, The Blues Agosti 2 katika mchezo wa Ngao ya Jamii.
  Petr Cech akiwa na jezi ya Arsenal baada ya kusaini kutoka Chelsea PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENE WENGER AFANYA KWELI, SASA PETR CECH NI KIPA WA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top