• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 28, 2015

  ENGLAND WAWEKA REKODI MPYA SOKA LA WANAWAKE, WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA

  TIMU ya taifa ya wanawake ya England imeweka rekodi ya kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yake, kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Canada usiku wa kuamkia leo Uwanja wa BC Place mjini Vancouver, Canada.
  England walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Jodie Taylor dakika ya 11 kabla ya Lucy Bronze kufunga la pili dakika tatu baadye, wakati bao la kufutia machozi la Canada lilifungwa na Christine Sinclair dakika ya 42.
  Kikosi cha Mark Sampson sasa kitamenyana na mabingwa watetezi Japan Jumatano katika Nusu Fainali Uwanja wa Commonwealth, Edmonton. Japan waliifunga 1-0 Australia jana bao pekee la Iwabuchi dakika ya 87.
  Nusu fainali ya pili itaikutanisha Ujerumani walioitoa Ufaransa kwa penalti 5-4 baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Marekani walioitoa China kwa bao 1-0 la Lloyd dakika ya 51 Uwanja wa Lansdowne, Ottawa.
  Kikosi cha England kilikuwa: Bardsley/Chamberlain dk50, Bronze, Houghton, Bassett, Rafferty, Moore, Williams/White dk79, Jill Scott, Chapman, Taylor na Carney/Stoney dk93. 
  Canada: McLeod, Wilkinson/Matheson dk62, Buchanan, Sesselmann, Chapman, Lawrence, Scott/Kyle dk77, Schmidt, Tancredi/Leon dk72, Belanger na Sinclair. 
  England players flock to Lucy Bronze (No 12) after her second goal in as many games put England in a commanding position 
  Wachezaji wa England wakimpongeza Lucy Bronze (jezi namba 12) baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Canada  PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ENGLAND WAWEKA REKODI MPYA SOKA LA WANAWAKE, WATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top