• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 30, 2015

  SIMBA SC YAZUIA JARIBIO LA BANDA KUTIMKIA YANGA, HANS POPPE ‘AMJAZA’ MAMILIONI LEO

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC imelazimika kumtimizia mahitaji yote kiungo Abdi Banda ili kuzuia mpango wa kuhamia kwa watani wa jadi, Yanga SC.
  Mapema leo, Banda alifika ofisini kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe kuomba ruhusa ya kuhamia kwa watani, Yanga SC kwa madai Msimbazi hathaminiwi.
  Hata hivyo, Poppe alimbana mchezaji huyo kutaka kujua undani wa madai yake na akasema ni salio la fedha zake za usajili na kodi ya nyumba.
  Hans Poppe (kushoto) leo amezuia zoezi la Abdi Banda kuhamia kwa watani Yanga SC

  Papo hapo, Poppe alifungua droo yake na kutoa maburungutu ya fedha kumaliza matatizo yote ya Banda, kodi ya nyumba na salio la fedha zake za usajili.
  Alipoulizwa na BIN ZUBEIRY jioni ya leo kuhusu suala hilo, kwanza Poppe alistaajbu habari hizo kuvuja.
  “Umejuaje? Haya mambo yametokea ofisini kwangu leo na tulikuwa wawili tu, mimi na mchezaji, au yeye ndiye amekuambia?”alihoji Poppe.
  Poppe akasema kwamba Banda ni mchezaji wa Simba SC hadi mwaka 2017, kwani alisaini Mkataba wa miaka mitatu mwaka jana aliposajiliwa kutoka Coastal Union. 
  “Hakuna tena madai yoyote ya Banda hapa, sisi tunamdai huduma kwa miaka mitatu,”alisema Poppe.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAZUIA JARIBIO LA BANDA KUTIMKIA YANGA, HANS POPPE ‘AMJAZA’ MAMILIONI LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top