• HABARI MPYA

  Ijumaa, Juni 26, 2015

  ALIYEMTIA 'DOLE' NYUMA CAVANI 'AFUKUZWA' KLABU YA BUNDESLIGA

  KLABU ya Mainz imekasirishwa mno na tabia mbaya za beki wake, Gonzalo Jara wiki hii na haihitaji tena kuendelea kuwa naye msimu ujao.
  Beki huyo wa pembeni wa zamani wa West Brom amekuwa akichezea timu hiyo ya Bundesliga tangu aondoke The Hawthorns mwaka jana.
  Lakini klabu hiyo kwa sasa ipo tayari kumuuza Jara baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu katika michuano ya Copa America inayoendelea nchini kwao, Chile. 
  Gonzalo Jara looks over his shoulder ahead of training on Thursday amid the Copa America controversy
  Gonzalo Jara akiangalia bega lake wakati wa mazoezi Alhamisi baada ya mambo ya aibu aliyofanya kwenye Copa America
  Jara approached Cavani late in the game
  He appeared to stick his finger in the striker's bum
  Jara alimtia dole nyuma Edinson Cavani wakati wa mchezo dhidi ya Uruguay
  Jara then theatrically falls to the ground after a light flick in the face from the PSG striker
  Jara alizabwa kibao na mshambuliaji huyo wa PSG 
  Cavani was shown a red card for two yellows after abusing the referee's assistant and the flick at Jara
  Cavani alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kibao Jara

  Kamera zilimnasa beki huyo mwenye umri wa miaka 29 akimtia dole nyuma Edinson Cavani, Chile ikishinda 1-0 dhidi ya Uruguay katika Robo Fainali Copa America.
  Cavani alitolewa kwa kadi nyekundu na Jara ambaye hakuadhibiwa, baadaye alifungiwa kutocheza sehemu yote iliyobaki kwenye mashindano hayo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ALIYEMTIA 'DOLE' NYUMA CAVANI 'AFUKUZWA' KLABU YA BUNDESLIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top