• HABARI MPYA

  Jumanne, Juni 30, 2015

  VARGAS APIGA ZOTE MBILI CHILE IKICHINJA 2-1 NA KUTINGA FAINALI COPA AMERICA

  WENYEJI Chile wametinga fainali ya Copa America 2015 kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Peru usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Taifa mjini Santiago:
  Kwa ushindi huo, fainali Chile sasa itakutana na mshindi kati ya Argentina na Paraguay zinazomenyana usiku wa kuamkia kesho.
  Eduardo Vargas aliifungia bao la kwanza akimalizia krosi ya Alexis Sanchez dakika ya 42.
  Carlos Zambrano alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Charles Aranguiz.
  Bao la kujifunga la Gary Medel dakika ya 60 liliwapa matumaini wageni, kabla ya Vargas kuifungia la ushidi Chile dakika ya 64.
  Kikosi cha Chile kilikuwa; Bravo, Isla, Medel, Rojas, Albornoz/Mena dk46, Vidal, Diaz/D Pizarro dk46, Aranguiz, Valdivia/Gutierrez dk86, E Vargas na Sanchez. 
  Peru; Gallese, Advincula, Zambrano, Ascues, Vargas, Carrillo/C Pizarro dk73, Ballon, Lobaton/Yotun dk73, Cueva/Ramos dk27, Farfan na Guerrero.
  Eduardo Vargas aliefunga mabao yote mawili Chile ikishinda 2-1 dhidi ya Peru na kutinga fainali Copa America PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VARGAS APIGA ZOTE MBILI CHILE IKICHINJA 2-1 NA KUTINGA FAINALI COPA AMERICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top