• HABARI MPYA

  Jumatano, Juni 24, 2015

  COVENANT BANK YAOKOA JAHAZI TAIFA QUEENS, YAWAPA TIKEZI NA MILIONI 40 KUFANIKISHA SAFARI

  Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akiwaonesha waandishi wa habari (hawako pichani) moja kati ya tiketi 20 zilizotolewa na Benki hiyo kwa Chama cha Mchezo wa Pete Tanzania (CHANETA) ili kufanikisha safari ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Queens) kwenda nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki michuano ya mabingwa wa Afrika benki hiyo imetoa zaidi ya milioni arobaini ili kufanikisha safari hiyo, Pamoja nae katika picha ni Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Kibira, na nahodha wa timu hiyo Sophia Komba.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja (Katikati) Pamoja na Mwenyekiti wa CHANETA. Anna Kibira, Nahodha wa Taifa Queens, Sophia Komba, ( kushoto) Baraka Enock, Meneja Uendeshaji Covenant Bank, na Allen Allex wa Wizara ya Michezo kwa pamoja wakiwa wameshika tiketi za ndege zilizotolewa na Benki hiyo kwa timu ya Taifa ya mpira wa Pete (Taifa Queens) ili kufanikisha safari ya kwenda nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mabingwa wa Afrika Benki hiyo imetoa zaidi ya Milioni Arobaini.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akikabidhi tiketi za ndege kwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Mpira wa Pete Tanzania (Taifa Queens) wakati wa Hafla ya kutangaza udhamini wa benki hiyo ili kufanikisha safari ya kwenda nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mabingwa wa Afrika Benki hiyo imetoa zaidi ya Milioni Arobaini
  Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, akimkabishi tiketi ya ndege, nahodha wa Taifa Queens, Sophia Komba wakati wa hafla ya kutangaza udhamini wa benki hiyo ili kufanikisha safari ya timu ya Taifa (Taifa Queens) kwenda nchini Botswana kwa ajili ya kushiriki michuano ya Mabingwa wa Afrika Benki hiyo imetoa zaidi ya Milioni Arobaini
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: COVENANT BANK YAOKOA JAHAZI TAIFA QUEENS, YAWAPA TIKEZI NA MILIONI 40 KUFANIKISHA SAFARI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top