• HABARI MPYA

    Friday, June 26, 2015

    ABAJALO, ALLIANCE, MADINI SC ZAPANDA DARAJA LA PILI

    Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
    TIMU za Abajalo FC ya Tabora, Alliance FC (Mwanza), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Madini SC (Arusha), na Sabasaba United FC (Morogoro) ndizo timu zilizopanda kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016.
    Timu hizo zimepanda daraja baada ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) iliyomalizika hivi karibuni kwenye vituo vya Lindi, Manyara na Rukwa na kushirikisha jumla ya timu 27.
    SDL inayoshirikisha timu 24 zilizogawanywa katika makundi manne inatarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 17 mwaka huu. Ligi hiyo itachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini, na timu itakayoongoza kundi ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2016/2017.
    Kundi A lina timu za Abajalo FC (Tabora), Green Warriors (Dar es Salaam), Milambo FC (Tabora), Mvuvumwa FC (Kigoma), Singida United (Singida) na Transit Camp (Dar es Salaam) wakati Kundi B ni AFC (Arusha), Alliance FC (Mwanza), Bulyanhulu FC (Shinyanga), JKT Rwamkoma FC (Mara), Madini SC (Arusha) na Pamba SC (Mwanza).
    Timu za kundi C ni Abajalo FC (Dar es Salaam), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Cosmopolitan (Dar es Salaam), Kariakoo FC (Lindi), Mshikamano FC (Dar es Salaam) na Villa Squad (Dar es Salaam).
    African Wanderers ya Iringa, Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Mkamba Rangers (Morogoro), Sabasaba United FC (Morogoro), Town Small Boys (Ruvuma) na Wenda FC ya Mbeya ndizo zinazounda kundi D.
    Dirisha la usajili wa wachezaji limeshafunguliwa tangu Juni 15 mwaka huu, na litafungwa Agosti 6 mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ABAJALO, ALLIANCE, MADINI SC ZAPANDA DARAJA LA PILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top