• HABARI MPYA

  Jumapili, Juni 21, 2015

  MESSI AFIKISHA MECHI 100 ARGENTINA IKITINGA ROBO FAINALI COPA AMERICA

  TIMU ya taifa ya Argentina imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamaica usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi B michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile. 
  Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Gonzalo Higuain dakika ya 11 tu ya mchezo huo na sasa Argentina inakwenda Robo Fainali.
  Jamaica ambayo haijashinda mchezo wowote katika kundi hilo, tayari imeaga michuano hiyo. Lionel Messi aliyetimiza mechi 100 timu ya taifa, sasa anaweza kukutana na Ecuador, Peru au Venezuela katika Robo Fainali.
  Kikosi cha Argentina kilikuwa: Romero, Rojo, Garay, Demichelis, Zabaleta, Biglia, Pastore/Pereyra dk59, Mascherano, Higuain/Tevez dk72, Messi na Di Maria/Lamela dk84.
  Jamaica: Miller, Hector/Taylor dk71, Morgan, Laing/Dawkins dk71, Brown/Barnes dk78, McAnuff, Watson, Austin, Mariappa, Lawrence na McCleary.
  Messi is greeted by a wall of Jamaican defenders as Argentina look to double their advantage following Higuain's early breakthrough 
  Messi akitafuta maarifa ya kuwatoka wachezaji wa Jamaica katika mchezo huo  PICHA ZAIDI GONGA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MESSI AFIKISHA MECHI 100 ARGENTINA IKITINGA ROBO FAINALI COPA AMERICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top