• HABARI MPYA

    Sunday, June 14, 2015

    VANESSA MDEE, ALI KIBA WANG’ARA, TUZO ZA KILI 2015, DIAMOND ANYAKUA MBILI

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    MWANAMUZIKI Ali Kiba usiku wa jana ameng’ara katika tuzo za muziki Tanzania, maarufu kama tuzo za Kili, akijinyakulia tuzo tano ikiwemo ya mwimbaji bora wa kiume wa mwaka na ile ya mtumbuizaji bora wa kiume wa mwaka, wakati Diamond ameambulia tuzo mbili tu. 
    Tuzo zingine za Ali Kiba ni pamoja na wimbo bora wa Afro Pop, mtunzi bora wa Bongo Fleva. Diamond ameibuka katika video bora ya mwaka kupitia wimbo wake wa “Mdogo Mdogo” na wimbo bora wa Zouk Rhumba. Yamoto Band wamepata tuzo moja ya Kundi Bora la Bongo Fleva. Mwimbaji mwenye sauti tamu na mvuto wa kipekee, Christian Bella ametoka mtupu kwa kushindwa kuambulia tuzo hata moja. Tuzo za Kili zimetolewa Jumamosi usiku katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
    Vanessa Mdee akitumbuiza jana katika tuzo za Kili

    ORODHA KAMILI YA WASHINDI TUZO ZA 2015;
    1. Kikundi Bora cha Mwaka - Bongo Fleva - Yamoto Band
    2. Kikundi Bora cha Mwaka Taarab - Jahazi Modern Taarab
    3. Bendi Bora ya Mwaka - FM Academia
    4. Msanii Bora Chipukizi - Baraka Da Prince
    5. Wimbo Bora Wenye Vionjo Vya Asili Ya Kitanzania (Waite) -Mrisho Mpoto Ft. Felly Kano
    6. Wimbo Bora Wa Zouk/Rhumba - Nitampata Wapi - Diamond Platinumz
    7. Wimbo Bora Wa Afro Pop - Mwana Ali Kiba
    8. Video Bora Ya Mwanamuziki Ya Mwaka – Mdogo Mdogo - Diamond Platinumz
    9. Mtayarishaji Bora wa Mwaka Bendi - Enrico
    10. Mtayarishaji Bora wa Nyimbo wa Mwaka Bongo Fleva - Nahreel
    11. Mtunzi Bora wa Mwaka- Hip Hop - Joh Makini
    12. Mtunzi Bora wa Mwaka Bendi - Jose Mara
    13. Mtunzi Bora wa Mwaka Bongo Fleva - Ali Kiba
    14. Mtunzi Bora wa Mwaka Taarab- Mzee Yussuf
    15. Mtumbuizaji Bora wa Muziki Wa Mwaka Wa Kiume - Ali Kiba
    16. Mtumbuizaji Bora wa Muziki Wa Mwaka Wa Kike - Venessa Mdee
    17. Mwimbaji Bora wa Kiume Taarab - Mzee Yussuf
    18. Mwimbaji Bora wa Kiume Bongo Fleva - Ali Kiba
    19. Mwimbaji Bora wa Kike Taarab - Isha Mashauzi
    20. Mwimbaji Bora wa Kike Bongo Fleva - Vanessa Mdee
    21. Wimbo Bora wa Taarab (Mapenzi Hayana Dhamana)- Isha Mashauzi
    22. Wimbo Bora wa Mwaka (Mwana)- Ali Kiba
    23. Wimbo Bora wa Kiswahili Bendi (Walewale) -Vijana Wa Ngwasuma
    24. Wimbo Bora wa R&B (Siksikii)- Jux
    25. Rapa Bora Wa Hip Hop - Kipi Sijasikia ( Prof J Ft. Diamond Platinumz)
    26. Msanii Bora wa Hip Hop - Joh Makini
    27. Wimbo Bora wa Afrika Mashariki (Sura Yako) - Sauti Sol
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VANESSA MDEE, ALI KIBA WANG’ARA, TUZO ZA KILI 2015, DIAMOND ANYAKUA MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top