![]() |
| Malinzi akiwa amembeba Coutinho |
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi amesema mtoto Feisal Awadh Salum ana kipaji cha kipekee na kama atapata mwendelezo mzuri, atakuwa mchezaji mkubwa baadaye.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana baada ya fainali ya michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 13 jana, Malinzi amesema kwamba amevutiwa mno na kipaji cha kijana huyo.
“Kwa ujumla mashindano yalikuwa mazuri na vijana wameonyesha vipaji vya hali ya juu, hii ni kuashiria kwamba tutapa timu bora ya baadaye ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17,”amesema Malinzi.
Feisal ambaye wenzake wanamuita kwa jina la utani Coutinho, wakimfananisha na Mbrazil wa Yanga SC, Andrey Coutinho alifunga bao la tatu katika ushindi wa 3-2 wa Ilala dhidi ya Alliance Academy katika fainali jana Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Feisal pia alitoa pasi zote za mabao mengine ya Ilala yaliyofungwa na Morris Michael Njaku ‘Chuji’ aliyeibuka mfungaji bora wa mashindano kwa mabao yake tisa.
Kwa upande wake, Feisal amesema kwamba amefurahia kuiwezesha Ilala kuwa bingwa wa mashindano na anatarajia mafanikio zaidi.
“Nimefurahi tumekuwa mabingwa wa mashindano haya. Tulikuja huku kwa ajili ya kushindana ili tuwe mabingwa na tumefanikiwa,”amesema dogo huyo aliyezaliwa miaka 12 iliyopita.
Kiungo huyo mshambuliaji ni mkazi wa Ilala Sharrif Shamba, Dar es Salaam ambaye anasoma shule ya Msingi Msimbazi Mseto darasa la sita.
Mtoto huyo (mama) Tumaini William Lukuwi, mbali na kufunga mabao matatu katika mashindano hayo, pia ameongoza kwa kutoa pasi nyingi mabao, 10.
![]() |
| Feisal 'Coutinho' akiwa amebebwa juu na wenzake baada ya kuonyesha kiwango kikubwa Ilala ikiifunga 3-2 Alliance Academy katika fainali ya U13 |




.png)
0 comments:
Post a Comment