Na Omary Katanga, DAR ES SALAAM
CHAMA cha Soka Dar es Salaam (DRFA) kimesikitishwa na matokeo mabaya iliyoyapata timu ya taifa (Taifa Stars) kwa kufungwa mabao 3-0 dhidi ya Mafarao wa Misri,katika mchezo wake wa kwanza uliopigwa jana usiku ugenini wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya kuwania kombe la mataifa ya afrika (AFCON).
Mwenyekiti wachama hicho, Almasi Kasongo, amesema matokeo hayo yamewafadhaisha mno watanzania wenye uchu wa kuona timu hiyo inapata matokeo mazuri yaliyokosekana kwa kipindi kirefu.
Amesema anaamini kuwa kikosi hicho kina wachezaji wazuri na wenye uwezo, lakini wamekuwa wakikosa mbinu za kufanya vizuri kwenye timu ya taifa hasa kwenye safu ya ushambuliaji, ikilinganishwa na uwezo wanaouonyesha kwenye michuano ya ligi wakiwa na klabu zao.
Hata hivyo Kasongo amesema licha ya Stars kuanza vibaya katika harakati zake za kuwania tiketi yamichuano hiyo ya afrika, bado nafasi ipo ya kujipanga upya kwa kuanza kuangalia uwezo wa benchi la ufundi.
Aidha, amesema DRFA inaamini kuwa TFF ina uwezo wa kutafuta mwarobaini wa kutibu tatizo la matokeo mabaya kwa Stars, bila kumuonea mtu aibu.
Taifa Stars, inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imepoteza mchezo wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 - 0 na wenyeji Misri.
Taifa Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 - 0.
Kipindi cha pili Misri walifanya mabadiliko yaliyowapelekea kupata mabao hayo 3 ndani ya dakika 10, kupitia kwa Ramy Rabia(60), Basem Morsy(64) na Mohamed Salah (69).
Stars ilifanya mabadiliko ya kuwaingiza Frank Domayo, Saimon Msuva na Salim Mbdonde na kufanya shambulizi kadhaa langoni kwa Misri lakini mashambulzi hayo yaliokolewa na walinzi wa timu ya Misri.
Mara baada ya mchezo huo, Taifa Stars inaondoka leo Alexandria kuelekea Cairo ambapo itaondoka na shirika la ndege la Ethiopia saa 8 usiku na kufika jijini Dar es salaam jumanne saa 7 mchana.
Tanzania: Deogratias Munish, Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Aggrey Morris/Salim Mbonde, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto/Saimon Msuva, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samata, Amri Kiemba/Frank Domayo.
Misri: Ahmed El Shenawy, Ahmed Hegazy, Ramy Rabea, Mohamed Abd Elshafy, Hazem Emam, Mohamed Elneny, Ibrahim Salah, Mahmoud Abd Elmonem/Ramadan Soffiy, Mohamed Salah/Mostafa Ftahy, Doly Elgabay/Basem Morsy, Ahmed Hassan Meky.

.png)
0 comments:
Post a Comment