• HABARI MPYA

  Tuesday, December 16, 2014

  BABU MHOLANZI ATUA YANGA SC NA KUSEMA; “NDOTO ZIMETIMIA, SUBIRINI MAMBO”

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MHOLANZI Hans van der Pluijm amewasili Saa 8:30 usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya Shirika la Ethiopia tayari kurudi kazini Yanga SC.
  Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, Pluijm alisema amefurahi kurudi Yanga SC na hiyo inamaanisha ndoto zake zimetimia.
  “Nimefanya mazungumzo na Yanga, natarajia nitasaini Mkataba baadaye (leo), sasa nakwenda kupumzika kwanza,”alisema.
  Hans van der Pluijm baada ya kuwasili JNIA usiku wa kuamkia leo

  REKODI YA PLUIJM YANGA SC 

  Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki)
  Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki)
  Yanga SC 2-1 Ashanti United (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
  Yanga SC 5-2 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
  Yanga SC 7-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu ya Bara)
  Yanga SC 1-0 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa)
  Yanga SC 0-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa. Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)
  Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar  (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu)
  Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
  Yanga SC 5-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)
  Pluijm aliyepokewa na Meneja wa klabu hiyo, Hafidh Saleh amesema kwamba anaamini atafanya kazi nzuri na kuwafurahisha wapenzi wa timu hiyo ambao kiu yao ni ushindi na mataji. 
  Kuwasili kwa Pluijm maana yake ndiyo mwisho wa makocha Wabrazil, Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo waliofukuzwa rasmi jana.
  Mholanzi huyo atafanya tena kazi na aliyekuwa Msaidizi wake awali akifundisha Yanga SC, mzalendo, Charles Boniface Mkwasa.
  Maximo anaondolewa baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu Simba SC Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe.
  Mkwasa tayari alisaini Mkataba wiki kadhaa zilizopita na ameridhika kufanya kazi chini ya Pluijm tena.
  Maximo na Leonardo walitua Yanga SC Julai mwaka huu kurithi mikoba ya Pluijm na Mkwasa ambao walipata kazi Uarabuni. Hata hivyo baada ya muda usiozidi mwezi mmoja, Pluijm na Mkwasa waliacha kazi Uarabuni, wakidai kukerwa na kuingiliwa na viongozi wa klabu yao katika masuala ya kiufundi.
  Pluijm alirudi Ghana wakati Mkwasa alirejea nyumbani Tanzania kabla ya kuajiriwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama Mkufunzi Mkuu.
  Hadi anaondoka Yanga SC, Maximo ameiongoza timu hiyo katika mechi 14, kati ya hizo akishinda 10, sare moja na kufungwa tatu dhidi ya Kagera Sugar 1-0, Mtibwa Sugar 2-0 sawa na Simba SC katika Mtani Jembe.
  Pluijm akiwa kwenye gari kuelekea hotelini
  Pluijm aliiongoza Yanga SC katika mechi 19, akishinda 11, sare sita na kufungwa mbili dhidi ya Al Ahly 1-0 Cairo na Mgambo JKT 2-1 Tanga.
  Maximo alikuwa anafanya kazi kwa mara ya pili Tanzania, baada ya awali kuwa kocha wa timu ya soka ya taia, Taifa Stars kuanzia mwaka 2006 hadi 2010.Yanga SC ilikuwa tayari kuendelea na Maximo iwapo angekubali kufanya kazi na Mkwasa, lakini baada ya kukataa, klabu imeoana bora kuachana naye.

  REKODI YA MAXIMO YANGA SC

  Yanga SC 1-0 Chipukizi (kirafiki Pemba)
  Yanga 2-0 Shangani (kirafiki Zanzibar)
  Yanga SC 2-0 KMKM (Kirafiki Zanzibar)
  Yanga SC 1-0 Thika United (Kirafiki Taifa)
  Yanga SC 3-0 Azam FC (Ngao ya Jamii)
  Yanga SC 0-2 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-1 Prisons (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
  Yanga SC 0-0 SImba SC (Ligi Kuu)
  Yanga SC 3-0 Stand United (Ligi Kuu)
  Yanga SC 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-0 Express (Kirafiki, Taifa)
  Yanga SC 0-2 Simba SC (Nani Mtani Jembe)
  Matatizo; Kocha Marcio Maximo ameondolewa Yanga SC baada ya mechi 14, akifungwa tatu 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BABU MHOLANZI ATUA YANGA SC NA KUSEMA; “NDOTO ZIMETIMIA, SUBIRINI MAMBO” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top