• HABARI MPYA

    Sunday, April 12, 2026

    AZAM FC NAYO YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB, YAIPIGA FOUNTAIN GATE 4-0


    TIMU ya Azam FC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate FC jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
    Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jephte Kitambala Bola dakika ya 15, winga wa kulia Mnigeria, Abel Abah dakika ya 21 na wazawa, beki wa kulia Ashrafu Shabani Kibeku dakika ya 81 na mshambuliaji, Alobogast Charles Kyobya dakika ya 90’+1.
    Azam FC inakamilisha idadi ya timu nane za Robo Fainali ya Kombe la CRDB, nyingine ni Simba SC, Singida Black Stars, TRA United, Coastal Union, JKT Tanzania, Mashujaa FC na mabingwa watetezi, Yanga SC.
    MATOKEO NA RATIBA 16 BORA KOMBE LA CRDB
    Azam FC 4-0 Fountain Gate
    Namungo FC 0-2 TRA United
    Simba SC 3-1 Dodoma Jiji 
    Singida Black Stars 5-1 Mbeya City
    Yanga SC 1-0 TMA Stars 
    Coastal Union 2-0 Pamba Jiji FC
    JKT Tanzania 3-0 Mbuni FC
    Geita Gold 0-0 Mashujaa FC (Penalti 2-4)

    Next
    This is the most recent post.
    Older Post
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC NAYO YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CRDB, YAIPIGA FOUNTAIN GATE 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top