• HABARI MPYA

    Saturday, April 11, 2026

    COASTAL UNION NAYO YATINGA NANE BORA KOMBE LA CRDB



    TIMU ya Coastal Union imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB  baada ya kuwatoa wapinzani wao wa Ligi Kuu, Pamba Jiji FC jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Mabao ya Coastal Union yamefungwa na kiungo mshambuliaji, Lassa Gradi Kiala dakika ya 30 na beki Ally Ayubu Msangi 'Zonzi' dakika ya 35.
    Coastal Union inaungana na timu nyingine mbili za Ligi Kuu, JKT Tanzania na Mashujaa FC zilizotangulia Robo Fainali ya Kombe la CRDB jana baada ya kuzitoa  timu za Ligi ya Championship leo.
    Wakati JKT Tanzania iliitupa nje Mbuni FC ya Arusha kwa kuichapa 3-0, mabao ya Edward Songo na Anuar Kilemile Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam - Mashujaa FC iliitoa Geita Gold kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila mabao Uwanja wa Sekondari ya Nyankumbu, Geita.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION NAYO YATINGA NANE BORA KOMBE LA CRDB Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top