MABINGWA watetezi, Yanga SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TMA ya Arusha jioni ya leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Shujaa wa Yanga SC leo ni kiungo mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Maxi Mpia Nzengeli aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 69 akimalizia pasi ya kiungo mwingine, Edmund John..
Yanga inakuwa timu ya tatu kwenda Robo Fainali ya Kombe la CRDB baada ya Coastal Union iliyoitoa Pamba Jiji FC jioni ya leo kwa kuichapa 2-0 Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga, mabao ya kiungo mshambuliaji, Lassa Gradi Kiala dakika ya 30 na beki Ally Ayubu Msangi 'Zonzi' dakika ya 35.
Timu nyingine mbili za Ligi Kuu, JKT Tanzania na Mashujaa FC zilitangulia Robo Fainali ya Kombe la CRDB jana kwa kuzitoa timu za Ligi ya Championship leo.
Wakati JKT Tanzania iliitupa nje Mbuni FC ya Arusha kwa kuichapa 3-0, mabao ya Edward Songo na Anuar Kilemile Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam - Mashujaa FC iliitoa Geita Gold kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila mabao Uwanja wa Sekondari ya Nyankumbu, Geita.

.png)
0 comments:
Post a Comment