• HABARI MPYA

  Tuesday, December 16, 2014

  EVERTON YAIFUMUA 3-1 QPR LIGI KUU ENGLAND

  KLABU ya Everton imeifumua mabao 3-1 Queens Park Rangers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana.
  Ross Barkley alifunga bao la kwanza dakika ya 33 kabla ya Kevin Mirallas kufunga la pili dakika 10 baadaye na Steven Naismith kufunga la tatu dakika ya 53.
  Bobby Zamora aliyetokea benchi aliifungia QPR bao la kufutia dakika ya 80 machozi na sasa kikosi cha Roberto Martinez kinapanda juu ya mahasimu wao wa nyumbani, Liverpool katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
  Ross Barkley opens the scoring with a wonder goal from distance in Everton's 3-1 victory against QPR
  Ross Barkley akiifungia bao la kwanza Everton katika ushindi wa 3-1 dhidi ya QPR 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EVERTON YAIFUMUA 3-1 QPR LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top