• HABARI MPYA

  Sunday, December 14, 2014

  AMIR KHAN AMTWANGA DEVON, SASA AJIWEKA ANGA ZA MAYWEATHER

  BONDIA Muingereza mwenye asili ya India, Amir Khan amemshinda kwa pointi mpinzani wake Devon Alexander katika pambano la raundi 10 uzito wa Welter Alfajiri ya leo ukumbi wa MGM Grand, las Vegas, Marekani.
  Khan alimzidi mno mpinzani wake huyo na kutawala raundi zote na kwa kiwango hicho amejitengenezea mazingira ya kuzipiga na Floyd Mayweather mwakani.
  Khan alirusha jumla ya ngumi 563 dhidi ya 461 za mpinzani wake, huku 243 zikimfika vyema Devon aliyefanikiwa kufikisha makonde 91 pia kwa Muhindi huyo.
  Wengi wanaamini Khan atakuwa mpinzani sahihi ajaye wa Mayweather kufuatia kumpiga bingwa wa dunia mara tatu, Devon. Mayweather amekwishasema atapigana na Manny Pacquiao Mei 1 mwakani, lakini kuna uwezekano akaanza Khan.   
  Amir Khan holds up a belt after defeating Devon Alexander
  Amir Khan akimtupia konde Alexander (kushoto) na kulia akishangilia na promota Oscar de la Hoya (kulia)
  Time and time again, Khan was first with the jab as he opened up a healthy lead over Alexander
  Khan akimuadhibu Alexander

  PICHA ZAIDI NENDA: http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-2873119/Amir-Khan-dominates-Devon-Alexander-Las-Vegas-Brit-face-Floyd-Mayweather-Jr.html#ixzz3LrrypmNU 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AMIR KHAN AMTWANGA DEVON, SASA AJIWEKA ANGA ZA MAYWEATHER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top