TIMU za Ligi Kuu, JKT Tanzania na Mashujaa FC zimefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kuzitoa timu za Ligi ya Championship leo.
JKT Tanzania imeitupa nje Mbuni FC ya Arusha kwa kuichapa 3-0, mabao ya Edward Songo na Anuar Kilemile Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Nayo Mashujaa FC imeitoa Geita Gold kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya bila mabao Uwanja wa Sekondari ya Nyankumbu, Geita.



.png)
0 comments:
Post a Comment