Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC inaingia kambini katika hoteli ya Valley View, Mtaa wa Kongo, Kariakoo, Dar es Salaam jirani kabisa na makao makuu yao, Jangwani kujiandaa na mchezo dhidi ya Mgambo JKT Jumamosi.
Yanga watakuwa wenyeji wa Mgambo katika mfululizo wa Ligi Kuu keshokutwa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakihitaji pointi tatu za kujiweka sawa kwenye mbio za ubingwa.
Yanga SC ambayo mchezo wake uliopita ilifungwa 1-0 na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba imekuwa ikiendelea na mazoezi Uwanja wa sekondari ya Loyola, Dar es Salaam tangu irejee Jijini mwanzoni mwa wiki.
Beki na Nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro' anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu na mshambuliaji majeruhi, Hussein Javu ndiyo wachezaji pekee ambao hawataingia kambini jioni hii, lakini winga Simon Msuva aliyekuwa majeruhi kwa wiki mbili zilizopita, yuko fiti naye anaingia kambini.
Msuva aliyekuwa anasumbuliwa na maumivu ya kiuno, amefanya mazoezi kikamilifu na wenzake kwa siku ya pili leo na anaonekana kuwa fiti kwa asilimia 100.
Yanga SC inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 10 sawa na Azam FC iliyo nafasi ya pili kwa wastani wa mabao, Coastal Union pointi 11 na Mtibwa Sugar wenye pointi 14 kileleni.
Kocha, Marcio Maximo atamkosa Msaidizi wake, Mbrazil mwenzake, Leonardo Leiva katika benchi Jumamosi baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi na Kagera Jumamosi iliyopita.

![]() |
| Kikosi cha Yanga SC 2014 |

.png)
0 comments:
Post a Comment