• HABARI MPYA

    Thursday, November 06, 2014

    IRAN WAKATAA KUGEUZWA ‘BUZI’ NA KENYA KISA MECHI NA HARAMBEE STARS

    Na Vincent Opiyo, NAIROBI
    TIMU ya taifa la Kenya, Harambee Stars imepigwa na butwaa baada ya Shirikisho la Soka Iran kutupilia mbali ombi lao la dola za Kimarekani 50,000 ili kusafiri nchini humo kwa mechi ya kirafiki Novemba 14.
    Inadaiwa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) liliitaka Iran itoe dola 50,000 mbali na gharama usafiri na malazi ya kikosi hicho cha Harambee Stars, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na rais wa Shirikisho la Iran Ali Kaffashian.
    “Shirikisho la soka nchini Kenya limeomba dola za marekani 50, 000 pamoja na gharama za usafiri na malazi yao, lakini kwetu hilo ni jambo geni kwa taifa ambalo lipo nafasi ya 116 kwenye orodha ya FIFA”, Kaffashian aliliambia Shanghai Daily.

    Kwa mujibu wa Kaffashian, itawalazimu kutafuta nchi nyingine barani Afrika ili kuchuana nao wakati wa wiki ya FIFA.
    Kenya imekuwa na mazoea ya kulamba hela za nchi za Uarabuni kwa kisizingizio kuwa wanamenyana nao kwenye mechi za kirafiki.
    Katika mechi za awali, Kenya ilipigwa 1-0 na Misri Uwanja wa Aswan Agosti kabla ya kuzabwa 3-0 na Morocco Oktoba mjini Marrakech.
    Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Kenya, Robert Asembo hakupokea simu zetu kuthibitisha taarifa hizi na iwapo Kenya itashiriki mechi ya kirafiki wakati huo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: IRAN WAKATAA KUGEUZWA ‘BUZI’ NA KENYA KISA MECHI NA HARAMBEE STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top