• HABARI MPYA

    Wednesday, August 20, 2014

    MAN UNITED YAFANYA KWELI, YAMTIA MIAKA MITANO ROJO NA KUMPA JEZI NAMBA 5

    KLABU ya Manchester United imethibitisha kumsajili beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo kwa dau la Pauni Milioni 16.
    Rojo, aliyetua Manchester jana na kusema 'anahisi kama ndoto', amesaini Mkataba wa miaka minne baada ya kufuzu vipimo vya afya na kuafiki vipengele vya mkataba binafasi.
    Louis van Gaal aliamua kutoa kipaumbele usajili wa beki huyo mtumia mguu wa kushoto, Rojo mwenye umri wa miaka 24, kufuatia kuanza vibaya Ligi Kuu ya England kwa kufungwa mabao 2-1 nyumbani na Swansea. Muargentina huyo atavaa jezi namba tano.

    Rojo ni Mwekundu: Manchester United hatimaye imekamilisha usajili wa Marcos Rojo kutoka Sporting Lisbon
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MAN UNITED YAFANYA KWELI, YAMTIA MIAKA MITANO ROJO NA KUMPA JEZI NAMBA 5 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top