• HABARI MPYA

  Sunday, August 31, 2014

  ARSENAL YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA LEICESTER CITY

  ARSENAL imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 ugenini na Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo.
  Alexis Sanchez alitangulia kuifungia Arsenal dakika ya 20, kabla ya Leonardo Ulloa kuisawazishia Leicester dakika mbili baadaye. 
  Ulloa na Jamie Vardy walipoteza nafasi nzuri za kuifungia Leicester kwenye mchezo huo, wakati upande wa Arsenal napo, Aaron Ramsey na Yaya Sanogo nao walikosa ya mabao ya wazi.
  Alexis Sanchez aliifungia bao la kuongoza Arsenal leo

  Kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Koscielny/Chambers dk26, Monreal, Ramsey, Flamini, Sanchez, Ozil/Cazorla/Chamberlain dk77, Sanogo/Podolski dk77.
  Leicester: Schmeichel, De Laet, Morgan, Moore, Konchesky, Mahrez/Albrighton dk65, Hammond, King, Schlupp/Vardy dk70, Ulloa na Drinkwater.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YALAZIMISHWA SARE 1-1 NA LEICESTER CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top