• HABARI MPYA

  Wednesday, August 27, 2014

  BARCA TAYARI KUSAINI BEKI LA KUSHAMBULIA LA KIBRAZIL

  KLABU ya Barcelona imekubali kumsajili beki wa kulia Douglas Pereira kutoka Sao Paulo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 3.19, vigogo hao wa Katalumya wamethibitisha jana.
  Uhamisho unaweza kupanda kwa Pauni Milioni 1.2 zaidi kwa ajili ya beki huyo mwenye umri wa miaka 24 kulingana idadi ya mechi atakazocheza katika klabu yake mpya.
  Pereira atajiunga na klabu hiyo ya La Liga kwa mkataba wa miaka mitano iwapo atafaulu vipimo vya afya wiki hii nchini Hispania.

  Beki la kushambulia: Beki huyo amefunga mabao sita katika mechi 124 alizoichezea Sao Paulo miaka mitatu iliyopita
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCA TAYARI KUSAINI BEKI LA KUSHAMBULIA LA KIBRAZIL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top