• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 31, 2014

  LIVERPOOL YAUA 3-0 BALOTELLI AKIANZA BILA BAO

  LIVERPOOL imeichapa mabao 3-0 Tottenham Hotspur katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa White Hart Lane.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya nane kwa shuti la umbali wa mita saba, Steven Gerrard dakika ya 48 kwa penalti baada ya Eric Dier kumchezea rafu Joe Allen na Alberto Moreno dakika ya 60.
  Liverpool imeng'ara leo kutoka kulia Sturridge, Gerrard na Balotelii

  Mshambuliaji mpya, Mario Balotelli aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 16 kutoka AC Milan wiki iliyopita, leo amecheza mechi yake ya kwanza Liverpool, lakini hakufunga licha ya kucheza soka nzuri.
  Kikosi cha Liverpool kilikuwa; Mignolet, Manquillo, Moreno, Gerrard, Lovren, Sakho, Henderson, Sterling/Enrique dk86, Sturridge, Balotelli/Markovic dk61 na Allen/Can dk61.
  Tottenham Hotspur: Lloris, Dier, Rose/Davies dk72, Capoue, Kaboul, Vertonghen, Lamela, Bentaleb/Dembele dk59, Adebayor, Eriksen/Townsend dk59 na Chadli.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAUA 3-0 BALOTELLI AKIANZA BILA BAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top