• HABARI MPYA

  Wednesday, August 27, 2014

  SIMBA SC YAMTEMA BEKI MRUNDI WA DJIBOUTI, DON MOSOTI KUENDELEA KULA MAISHA MSIMBAZI

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  BEKI Hussein Butoyi hajamvutia kocha Patrick Phiri na Simba SC imeamua kuachana naye- maana yake Mkenya Donald Mosoti amenusurika kupigwa panga.
  Mrundi huyo alimvutia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe akiichezea Telecom ya Djibouti katika Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda mwezi huu.
  Poppe akafanya mazungumzo na mchezaji huyo aje Dar es Salaam kufanya majaribio na kama angemvutia kocha Mzambia, angepewa mkataba.
  Anarudi Djibouti; Hussein Patiyo hatasajiliwa Simba SC baada ya kushindwa kumvutia kocha Patrick Phiri 

  Hata hivyo, baada ya wiki moja ya kufanya mazoezi na Simba SC visiwani Zanzibar pamoja na kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Kilimani City, kiwango chake hakijamvutia kocha Phiri.
  Wakati dirisha la usajili la Simba SC linafungwa usiku wa leo, Kamati ya Usajili kwa pamoja na Kamati ya Ufundi zimeafikiana kuachana na Butoyi na kuendelea na Mosoti.
  Maana yake wachezaji wa kigeni katika kikosi cha Simba SC watakuwa mabeki Mganda Joseph Owino, Mkenya Mosoti, Warundi kiungo Pierre Kwizera, mshambuliaji Amisi Tambwe na Mkenya Mkenya Paul Kiongera. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAMTEMA BEKI MRUNDI WA DJIBOUTI, DON MOSOTI KUENDELEA KULA MAISHA MSIMBAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top