• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 30, 2014

  CHUJI: BADO SIONI MIDO KAMA MIMI NCHI HII

  Na Dina Ismail, DAR ES SALAAM
  KIUNGO Athumani Iddi ‘Chuji’ amesema kwamba bado haoni kiungo mwenye uwezo kama wake kwa sasa nchini na japokuwa hajasaini timu yoyote hadi sasa, lakini anaamini atarudi vizuri kazini muda si mrefu.
  “Sijasaini timu yoyote, hata hizi habari za mimi kusaini Mwadui, nashangaa sijui zinatoka wapi, ila tulia ndugu yangu, muda si mrefu nitarudi kazini na wananchi watafurahi,”amesema Chuji akizungumza na BIN ZUBEIRY jana.
  Hakuna kama yeye; Athumani Iddi 'Chuji' amesema hajasaini Mwadui, lakini atarudi kazini muda si mrefu

  Kiungo huyo amesema kwa sasa anafanya mazoezi kama kawaida kuhakikisha anakuwa fiti muda wote akitakiwa kurejea kazini awe vizuri.
  “Ninaendelea na mazoezi, ilikuwa nisaini Azam lakini kuna mambo hayakwenda sawa, sikusaini. Timu nyingine kadhaa zilinifuata, lakini hatukuafikiana kwenye maslahi na sikuona sababu ya kufanya papara,”ameongeza Chuji.
  Chuji hakutaka kuongeza Mkataba Yanga SC baada ya msimu uliopita kutokana na kutofautiana na aliyekuwa kocha Msaidizi wa timu hiyo wakati huo, Charles Boniface Mkwasa.
  Hata hivyo, siku chache baada ya Chuji kuamua kujitoa Yanga SC, Mkwasa naye akaondoka timu hiyo kwenda kufundisha Uarabuni, ambako pia hakudumu na sasa amarejea nchini.
  Kwa sasa Yanga SC ipo chini ya makocha Wabrazil, Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Leiva.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHUJI: BADO SIONI MIDO KAMA MIMI NCHI HII Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top