• HABARI MPYA

  Thursday, August 28, 2014

  TANZANIA YAKWAMA UENYEJI AFCON, YAPAMNANA CAF IONDOE KIPENGELE KINACHOWAKWAMISHA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeliandikia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kutaka kipengele cha kutaka kwanza nchi iandae Fainali za Afrika kwa Vijana ndiyo iwe na sifa ya kuandaa Fainali za Afrika (AFCON) kiondolewe.
  TFF ilishapeleka barua CAF kutaka kipengele hicho kiondolewe, na kutaka kijadiliwe katika Congress (Mkutano Mkuu) ijayo ya CAF.
  Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inayowania ueyeji wa AFCON ya 2017

  Tanzania imeshaiandikia CAF barua kuomba uenyeji wa Fainali za AFCON za 2017 baada ya Libya iliyokuwa imepewe uenyeji huo kujitoa. Uamuzi wa Tanzania kuomba kuandaa fainali hizo ulifanywa na Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA YAKWAMA UENYEJI AFCON, YAPAMNANA CAF IONDOE KIPENGELE KINACHOWAKWAMISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top