• HABARI MPYA

  Saturday, August 30, 2014

  BREAKING NEWS; SIMBA YAMTEMA MOSOTI, YASAJILI KINDA LA ZANZIBAR HEROES

  Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
  SIMBA SC imefikia uamuzi wa kumtema beki Mkenya, Donald Mosoti na kumsajili beki chipukizi wa timu ya taifa ya Zanzibar, Shaffi Hassan ambaye msimu uliopita aliichezea Ashanti United katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Beki huyo wa kati kinda aliyekuwa akimuweka benchi mkongwe Vicotr Costa mbele ya kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ amesaini Mkataba wa miezi sita jana visiwani Zanzibar.
  Amemfuata kocha wake; Donald Mosoti (katikati) ametemwa. Kulia ni kocha Mcroatia Zdravko Logarusc aliyetimuliwa na kushoto kipa Ivo Mapunda, ambao kwa pamoja watatu hao walijiunga na Simba SC Desemba mwaka jana kutoka Gor Mahia ya Kenya

  Jana hiyo hiyo jina lake limetumwa kwenye usajili wa Simba SC na kuwahi kabla ya dirisha kufungwa.
  Hatua ya Simba SC kumkata beki huyo mrefu inafuatia kumsajili mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi ambaye klabu yake, Yanga SC inadai haijamuacha na bado ina mkataba naye. 
  Simba SC imelazimika kukata mgeni mmoja, Mosoti ili ibaki na wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni baada ya kumsajili na Okwi. Wengine ni Mganda, Joseph Owino, Warundi, Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Mungai Kiongera. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BREAKING NEWS; SIMBA YAMTEMA MOSOTI, YASAJILI KINDA LA ZANZIBAR HEROES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top