• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 28, 2014

  SANCHEZ AIPELEKA ARSENAL MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA

  BAO pekee la Alexis Sanchez limeipa ushindi wa 1-0 Arsenal katika mchezo wa marudiano hatua ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa Uwanja wa Emirates usiku huu.
  Kwa matokeo hayo, timu ya Arsene Wenger inasonga mbele hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 1-0, baada ya sare ya 0-0 awali katika mchezo wa kwanza Uturuki.
  Wenyeji walilazimika kucheza pungufu ya mchezaji mmojka kwa dakika 15 za mwisho, baada ya 
  Sanchez kulia akishangilia baada ya kuifungia Arsenal bao muhimu usiku huu Emirates

  Matheiu Debuchy kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano.
  The Gunners wanakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 17 mfululizo baada ya ushindi huo.
  Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Flamini, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Wilshere, Ozil/Chambers dk76 na Sanchez.
  Besiktas: Zengin, Koybasi, Franco, Gulum, Motta, Hutchinson, Ozyakup, Kavlak/Uysal dk76, Pektemek/Tosun dk87, Ba, Sahan/Tore dk60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SANCHEZ AIPELEKA ARSENAL MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top