• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 27, 2014

  ETO'O ATUA EVERTON KUMALIZIA SOKA YAKE MIAKA MIWILI

  KLABU ya Everton imetangaza kumsajili mshambuliaji Mcameroon, Samuel Eto'o kwa mkataba wa miaka miwili kama mchezaji huru.
  Mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 33 alitemwa na Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita na amejiunga na Toffees kufuatia mango wa kuhamia kwa majirani zao, Liverpool kukwama.
  Liverpool ilitaka kumsajili Eto'o iwapo ingemkosa Mario Balotelli, lakini baada ya kumnasa Mtaliani huyo, dili hilo limekufa kifo cha kawaida.
  Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona ametweet; "Rasmi ni mchezaji wa Everton...!!! Acha niwe tayari kwa matarajio na changamoto mpya!!!'  

  Anamwaga wino: Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Samuel Eto'o akisaini mkataba na Everton
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ETO'O ATUA EVERTON KUMALIZIA SOKA YAKE MIAKA MIWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top