• HABARI MPYA

  Sunday, August 31, 2014

  HII NDIYO 'FIRST ELEVEN' YA PHIRI SIMBA SC, HAKUNA OKWI, MKUDE WALA KIONGERA...NA BADO KUNA WAKALI WENGINE WA KIKOSI CHA PILI WANATISHA

  Hiki ndicho kikosi cha kwanza cha Simba SC, ambacho kocha Patrick Phiri amekuwa akikitanguliza dakika 45 za kwanza katika mechi zake visiwani Zanzibar. Na hiki ndicho kikosi kilichomaliza kipindi cha kwanza kinaongoza 4-0 dhidi ya KMKM jana katika ushindi wa 5-0. Kutoka kulia waliosimama ni Joram Mgeveke, Miraj Adam, Ivo Mapunda, Joseph Owino, Amri Kiemba, na Haroun Chanongo. Waliochuchumaa kutoka kulia ni Ramadhani Singano 'Messi', Pierre Kwizera, Shaaban Kisiga,  Amisi Tambwe na Issa Rashid. Wachezaji watatu wa kiwango cha juu, Emmanuel Okwi, Paul Kiongerea na Jonas Mkude hawapo hapa. Na kuna wachezaji wa kikosi cha pili kama Said Ndemla, Elias Maguri, Twaha Ibrahim 'Messi' wanafanya vizuri. Hii inamaanisha Simba SC ipo vizuri kuelekea msimu ujao.
  Kocha Patrick Phiri akiwa na Msaidizi wake, Suleiman Matola 'Osama' kushoto jana Uwanja wa Amaan

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HII NDIYO 'FIRST ELEVEN' YA PHIRI SIMBA SC, HAKUNA OKWI, MKUDE WALA KIONGERA...NA BADO KUNA WAKALI WENGINE WA KIKOSI CHA PILI WANATISHA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top