• HABARI MPYA

  Saturday, August 30, 2014

  COSTA MABAO APIGA MBILI CHELSEA IKICHAPA TIMU YA ETO'O SITA

  MSHAMBULIAJI Diego Costa, ameendelea kung’ara Chelsea baada ya leo kufunga mabao mawili katika ushindi wa 6-3 dhidi ya Everton Uwanja wa Goodison Park Ligi Kuu ya England.
  Costa alifunga sekunde ya 35 na dakika ya 90, wakati mabao mengine ya The Blues yalifungwa na Branislav Ivanovic dakika ya tatu, Coleman akajifunga dakika ya 67, Nemanja Matic dakika ya 74 na Ramires dakika ya 77.
  Samuel Eto’o aliifunga timu yake ya msimu uliopita inayofundishwa na kocha Mreno Jose Mourinho dakika ya 76, wakati mabao mengine ya Everton yamefungwa na Mirallas dakika ya 45 na Naismith dakika ya 69.
  Diego Costa kulia ameendelea kufanya vizuri Chelsea
  Kipa wa Everton, Tim Howard alinusurika kulimwa kadi nyekundu baada ya kudakia mpira nje ya eneo la penalti.
  Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian/Mikel dk75, Fabregas/Drogba dk89, Hazard/Luis dk83 na Costa.
  Everton: Howard, Coleman, Jagielka, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Naismith, McGeady/Eto'o dk70 na Lukaku/Besic dk89.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COSTA MABAO APIGA MBILI CHELSEA IKICHAPA TIMU YA ETO'O SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top