• HABARI MPYA

  Friday, August 29, 2014

  HATIMAYE TORRES AONDOKA CHELSEA, AENDA KUZIBA PENGO LA BALOTELLI AC MILAN

  HATIMAYE mshambuliaji Fernando Torres amemaliza miaka yake mitatu na nusu migumu Chelsea kwa kukubali kuhamia AC Milan.
  Mchezaji huyo wa Hispania anakwenda kuziba pengo la Mario Balotelli ambaye Milan imemuuza kwa Pauni Milioni 16 Mtaliano huyo Liverpool.
  Wakala wa Torres alifanya mazungumzo na Milan Alhamisi asubuhi na mshambuliaji huyo amekubali kujiunga na vigogo hao wa Italia kwa miaka miwili.
  Amechuja: Licha ya kusajiliwa kwa Pauni Milioni 50 kutoka Liverpool, Torres amemudu kufunga mabao 45 tu katika mechi 172 alizocheza Chelsea
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 anahamia San Siro kwa mkopo wa miaka miwili.
  Torres aliyetua Stamford Bridge kwa dau la Pauni Milioni 50 alikuwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake wa Pauni 150,000 kwa wiki Stamford Bridge na inaaminika wawakilishi wake walipatana kiasi hicho hicho cha mshahara kabla ya mchezaji huyo kukubali uhamisho huo. 
  Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho alikuwa radhi kumuacha Torres kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu ili kupata nafasi ya kusajili mshambuliaji mwingine na Loic Remy sasa yupo kwenye nafasi nzuri ya kutua Magharibi mwa London kutoka Queens Park Rangers.

  REKODI YA FERNANDO TORRES... 

  Atletico Madrid (2001-2007) Mechi 244, mabao 91
  Liverpool (2007-2011) Mechi 142, mabao 81
  Chelsea (2011-2014) Mechi 172, mabao 45
  Timu ya taifa Hispania tangu 2003; Mechi 110, mabao 38
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HATIMAYE TORRES AONDOKA CHELSEA, AENDA KUZIBA PENGO LA BALOTELLI AC MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top