• HABARI MPYA

    Friday, August 22, 2014

    JESHI JESHI TU MBELE YA POLISI…APR YATINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME, ITAMENYANA NA MERREIKH JUMAPILI AMAHORO

    Na Nagma Khalid, ZANZIBAR
    APR imefanikiwa kutinga Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuitoa Polisi, zote za hapa kwa penalty 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120.
    Kwa matokeo hayo, APR itakutana na El Merreikh ya Sudan katika Fainali Jumapili Uwanja wa Amahoro mjini hapa.
    Mikwaju ya penalty ya APR ilitiwa kimiani na Nshutinamagara Ismail, Mukunzi Yannick, Patrick Sibomana na Mugiraneza Baptiste, huku Eric Rutanga akikosa.

    Waliopata penalti za Polisi ni Jerome Sina na Moussa Habimana wakati Tuyisenge Jacqueline na Peter Kagabo.
    Polisi haikuweza kufua dafu kwa mikwaju ya penalti mbele ya APR, licha ya kuingiza kipa inayemuamini katika uchezaji michomo hiyo, Ntaribi Steven aliyekwenda kuchukua nafasi ya Marcelo Nzarora dakika mbili kabla ya filimbi ya mwisho.    
    Katika mchezo ulioangulia, Merreikh imekwenda Fainali kwa ushindi wa penalti 3-0, kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika 120.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JESHI JESHI TU MBELE YA POLISI…APR YATINGA FAINALI KOMBE LA KAGAME, ITAMENYANA NA MERREIKH JUMAPILI AMAHORO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top