• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 27, 2014

  KINDA WA MIAKA 42 WA CAMEROON ATUA FC BARI KWA MKOPO WA MWAKA MMOJA

  KIUNGO Joseph Minala wa Lazio ambaye aliwahi kufanyiwa uchuguzi wa umri wake ili kuthibitisha hana 42 akichezea timu ya vijana, amejiunga na FC Bari kwa mkopo wa mwaka mmoja.
  Minala anahamia klabu ya Daraja la Kwanza Italia, Serie B siku moja baada ya kutimiza miaka 18, akiwa amechezea mechi yake ya kwanza ya Serie A na Lazio msimu uliopita katika ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya Sampdoria.
  Na mzaliwa huyo wa Cameroon, Minala amesema; "Wamenipa umri tofauti, ukweli ni kwamba nina miaka 18. Mtu mmoja ametunga stori hii ambayo haikunugusa. Haijawahi kunisumbua kitu ambacho hakinuhusu,"amesema. 

  Uthibitisho: Joseph Minala amejiunga na FC Bari kwa mkopo wa mwaka mmoja baada ya kufikisha miaka 18
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KINDA WA MIAKA 42 WA CAMEROON ATUA FC BARI KWA MKOPO WA MWAKA MMOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top