• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 31, 2014

  SIMBA SC ILIVYOIFANYA KMKM JANA AMAAN

  Wachezaji wa Simba SC, Shaaban Kisiga kushoto na Pierre Kwizera kulia wakimpongeza mwenzao, Amri Kiemba baada ya kufunga bao la kwanza katika ushindi wa 5-0 jana dhidi ya KMKM katika mchezo wa kirafiki, Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
  Kiungo Pierre Kwizera akipasua katikati ya wachezaji wa KMKM
  Kiungo Shaaban Kisiga ambaye kwa sasa anachezeshwa kama mshambuliaji wa pili, akimtoka beki wa KMKM
  Mshambuliaji Elias Maguri akimiliki mpira mbele ya beki wa KMKM 
  Beki Issa Rashid 'Baba Ubaya' akimtoka beki wa KMKM 
  Kiungo wa pembeni wa Simba SC, Haroun Chanongo akitafuta mbinu za kumtoka beki wa KMKM
  Beki anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, William Lucian 'Gallas' akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa KMKM
  Kiungo Ibrahim Hajibu akijiandaa kumgeuza mchezaji wa KMKM
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC ILIVYOIFANYA KMKM JANA AMAAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top