• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 29, 2014

  MANJI: TUTASAJILI WA KIGENI SITA OKWI NA JAJA WOTE NDANI

  Na Samira Said, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imesema itatuma majina ya wachezaji sita wa kigeni katika usajili wao kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, badala ya watano wanaotakiwa kwa mujibu wa kanuni.
  Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Manji amewaambia Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani kwamba, jina la mshambuliaji Emmanuel Okwi kutoka Uganda litaongoza orodha hiyo.
  Mbali na Okwi, wachezaji wengine wa kigeni wa Yanga SC ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima kutoka Rwanda, Mganda Hamisi Kiiza na Wabrazil, Andrey Coutinho na Geilson Santana ‘Jaja’.
  Manji akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jangwani

  Lakini Okwi, pia amesajiliwa na Simba SC, maana yake usajili ya Mganda huyo utazua tafrani mbele ya safari.
  Dirisha la usajili kwa wachezaji wazalendo linatarajiwa kufungwa leo, baada ya Shirikisho la SOka Tanzania (TFF) kuongea siku mbili zaidi tangu juzi.
  Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa aliimbia BIN ZUBEIRY jana kwamba, sababu za kusogeza mbele ni klabu zote za Ligi Kuu kushindwa kukamilisha usajili juzi.
  “Nadhani wameshindwa kuutumia huu mfumo wetu mpya wa elektroniki, sasa tumewapa Saa 48 zaidi warekebishe, zikiisha hizo, hapo hakuna nafasi tena, tunasonga mbele,”amesema Mwesigwa jana.
  Amesema kwamba hadi muda wa kufunga usajili juzi Saa 6:00 usiku, ni timu moja tu, Kimondo FC ya Daraja la Kwanza ndiyo iliyokuwa imefanikiwa kukamilisha usajili wake katika mfumo huo. “Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Kimondo kwa kumudu kuutumia mfumo huu na kuwasilisha usajili wao ndani ya muda,”amesema. 
  Aidha, Mwesigwa amesema kwamba dirisha la usajili kwa wachezaji wa kigeni litafungwa Septemba 6, mwaka huu. “Hili dirisha la wachezaji wa kigeni likifungwa, hakuna nyongeza ya muda tena, kwa kuwa hili lipo katika mfumo wa kimataifa chini ya FIFA, likifungwa, limefungwa dunia nzima, hivyo nawasihi viongozi wa klabu wahakikishe hawafanyi makoasa,”amesema.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANJI: TUTASAJILI WA KIGENI SITA OKWI NA JAJA WOTE NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top