Kikosi cha KMKM kilichofungwa 5-0 na Simba SC jana katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Amaan, Zanzibar. KMKM pia ilikutana na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Azam FC ikafungwa 4-0 kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, au Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda. Ilikutana pia na Yanga SC Jumatano wiki hii katika mchezo wa kirafiki Amaan ikafungwa 2-0. KMKM ni mabingwa wa Zanzibar miaka miwili mfululizo. |
0 comments:
Post a Comment