• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 28, 2014

  RONALDO AMGARAGAZA TENA MESSI, ABEBA TUZO YA MWANASOKA BORA ULAYA

  MRENO Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya msimu wa 2013-2014 katika sherehe zilizofanyika jioni ya leo mjini Monaco, Ufaransa.
  Nyota huyo wa Real Madrid amewapiku nyota wa Bayern Munich, kipa Mjerumani Manuel Neuer na winga Mholanzi, Arjen Robben alioingia nao fainali. 
  Ronaldo akimkabidhi tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Rais wa Real Madrid, Perez 

  Wakati Neuer alishinda taji la Bundesliga na Kombe la Dunia msimu uliopita, Robben alifunga mabao 22 kwa klabu na timu yake ya taifa msimu uliopita na Ronaldo alifunga mabao 56 na kutoa pasi 15 za mabao Real Madrid na Ureno. Mshindi wa mwaka jana, Mfaransa Franck Ribery hakuingia fainali.
  Ronaldo pia ni Mwanasoka Bora wa Dunia na ushindi huu ni pigo lingine kwa mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Argentina na Barcelona.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AMGARAGAZA TENA MESSI, ABEBA TUZO YA MWANASOKA BORA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top