• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 26, 2014

  MAN CITY YAIFUMUA LIVERPOOL 3-1 ETIHAD

  MABINGWA wa Ligi Kuu ya England, Manchester City wamewachapa mabao 3-1 wapinzani wao katika mbio za taji hilo msimu uliopita, Liverpool usiku huu Uwanja wa Etihad mjini Manchester.
  Stevan Jovetic alifunga mabao mawili moja kila kipindi la kwanza dakika ya 41 na pili dakika ya 55 kabla ya Edin Dzeko kuingia na kufunga la tatu katika mpira wa kwanza aliogusa dakika ya 68.
  Dzeko alifunga bao hilo kabla hata Sergio Aguero aliuemposha hajafika kwenye benchi na Liverpool wakapata bao la kufutia machozi dakika ya 83 kupitia kwa Lambert. Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Mario Balotelli alikuwa jukwaani akiishuhudia timu yake ya zamani ikishinda. 

  Shujaa; Stevan Jovetic akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Manchester City bao la kwanza usiku huu

  Kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Clichy, Nasri, Toure, Fernando, Silva/Jesus Navas DK65, Jovetic/Fernandinho DK80 na Dzeko/Aguero dk69.
  Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Lovren, Moreno, Henderson, Gerrard, Allen/Can dk75, Sterling/Lambert dk79, Sturridge na Coutinho/Markovic dk60.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAN CITY YAIFUMUA LIVERPOOL 3-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top