• HABARI MPYA

  Sunday, August 31, 2014

  IMETIMIA MIAKA 10 ROONEY MCHEZAJI WA MAN UNITED

  MSHAMBULIAJI Wayne Rooney leo ametimiza miaka 10 tangu asajiliwe na Manchester United kutoka Everton.
  Rooney amepata mafanikio ya kuridhisha akiwa na United, ikiwemo kushinda mataji matano ya Ligi Kuu, moja la Ligi ya Mabingwa, moja la Klabu Bingwa ya Dunia na mawili ya Kombe la Ligi.
  Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Seri Alex Ferguson  kwa Pauni Milioni 25 Agosti 31, mwaka 2004 amefunga mabao 218 katika mechi 444 ndani ya miaka yake 10 kwenye klabu hiyo na sasa amepewa Unahodha na kocha mpya, Louis Van Gaal.

  Muongo mmoja: Wayne Rooney (kulia) ametimiza miaka 10 tangu asajiliwe Manchester United kutoka Everton Agosti 2004
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IMETIMIA MIAKA 10 ROONEY MCHEZAJI WA MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top