• HABARI MPYA

  Sunday, August 24, 2014

  MAN UNITED YAANZA KUJITAHIDI, YAPATA SARE NA SUNDERLAND UGENINI

  KOCHA Louis Van Gaal kwa mara nyingine ameshindwa kuipa ushindi Manchester United baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Sunderland Uwanja wa Light katika mchezo wa Ligi Kuu ya England. 
  Juan Mata alitangulia kuifungia United dakika ya 17, lakini Jack Rodwell akaisawazishia Black Cats dakika ya 30. Robin van Persie alirejea kwenye kikosi cha Mashetani Wekundu leo kwa mara ya kwanza tangu baada ya Kombe la Dunia, lakini akashindwa kuibeba timu hiyo.
  Hali tete; Wachezaji wa Manchester United, kutoka kulia Wayne Rooney, Juan Mata na Robin van Persie wakiwa hawaamini macho yao baada ya Sunderland kusawazisha bao

  Kikosi cha Sunderland kilikuwa; Mannone, Vergini, O'Shea, Brown, Van Aanholt, Larsson, Cattermole, Rodwell/Gomez dk63, Buckley/Bridcutt dk79, Fletcher/Altidore dk76 na Wickham. 
  Manchester United: De Gea, Jones, Smalling/Michael Keane dk44, Blackett, Valencia, Fletcher/Januzaj dk64, Cleverley, Young, Mata, Van Persie/Welbeck dk64 na Rooney. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAANZA KUJITAHIDI, YAPATA SARE NA SUNDERLAND UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top